Habari

Usimamizi wa Hospitali kuu ya Malindi Kaunti ya Kilifi umeeleza kutopokea fedha zilizotajwa kutengwa na Wizara ya afya Nchini…

Usimamizi wa Hospitali kuu ya  Malindi Kaunti ya Kilifi umeeleza kutopokea fedha zilizotajwa kutengwa na Wizara ya afya Nchini  kwa lengo la kuboresha vyumba vya wagonjwa mahututi pamoja na ununuzi wa vitanda vya wagonjwa wanaogua Covid-19.

Kulingana na msimamizi mkuu wa Hospitali hiyo Daktari Job Gayo, hospitali hiyo haijapokea  mgao huo licha ya Wizara ya Afya Nchini kudai kutenga kima cha Shillingi Billioni tano.

Afisa huyo sasa anaitaka Wizara ya Afya Nchini ifanye uchunguzi ili kubaini iwapo fedha hizo zilifikishwa katika hospitali husika huku akibainisha kuwa walipokea baadhi ya vifaa vya wahudumu vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Kwa upande mwengine, Gayo sasa anaitaka Serikali kuongeza vitanda vya wagonjwa wa Covid-19 katika Hospitali hiyo.

Daktari huyo ameongeza kuwa, Bado wanataka chumba cha wagonjwa mahututi wakati huu idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya Corona ikiongezeka kila uchao.