Habari

Jaji William Ouko asema suala la mrundiko wa kesi mahakamani atalipatia kipau mbele…

Rais wa mahakama ya rufaa jaji  William Ouko anahojiwa katika mahojiano ya kumtafuta jaji mkuu nchini.

Ouko amesema kwamba swala la kwanza ambalo atashughulikia ni swala  la mrundiko wa kesi mahakamani, akijibu swali la naibu jaji mkuu Philomena Mwilu, Ouko amesema kuwa mrundiko wa kesi mahakamani ni swala ambalo limekuwepo kwa muda.

Ouko aidha ameongeza kuwa ni haki ya kila mwananchi kupata huduma bora mahakamani.

Hata hivyo jaji Warsame amemtaka Ouko kueleza tatizo linaloikumba mahakama ya juu na iwapo atakuwa jaji mkuu atalishughulikia kwa jinsi gani kwa siku za kwanza sitini.

Ouko amesema kwamba ukosowaji wa mahakama umekuwepo kwa muda hivyo basi anahisi ni wakati mwafaka wa mahakama kutathmini tatizo hilo na pia kuwahusisha wasomi ili kutatua swala hilo