Wito umetolewa kwa madereva wanaotumia barabara ya Kombani-Kwale kuwa waangalifu na kuzingatia alama za barabarani ili kuzuia visa vya ajali za kiholela zinazoshuhudiwa.
Haya ni kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea jana asubuhi na watu watatu kufariki dunia baada ya kuhusika katika ajali hiyo katika eneo la Vuga kaunti ya Kwale.
Kamanda wa polisi kaunti hiyo Ambrose Oloo amethibitisha ajali hiyo kuwa mbaya iliyohusisha tuk tuk na lori ya kubeba mitungi ya gesi huku mtu mmoja alijeruhiwa vibaya.
Aidha, Kamanda huyo amewataka madereva wote wa tuk tuk, bodaboda, taxi na hata gari za umma wanaotumia barabara hiyo kuwa waangalifu zaidi na kuzingatia alama za barabarani sawia na kufuata sheria za trafiki kama njia ya kupunguza visa vya ajali barabarani