Habari

Polisi wanasa misokoto 550 ya bangi pamoja na kumnasa mshukiwa huyo wa ulanguzi wa mihadarati

Polisi mjini Malindi wamefaulu kunasa misokoto 550 ya bangi pamoja na kumnasa mshukiwa huyo wa ulanguzi wa mihadarati

Katika taarifa kwa wanahabari kamanda wa polisi kaunti ndogo ya malindi John Kemboi amesema kwamba maafisa wa upelelezi walipata taarifa kutoka kwa mmoja wa makachero wao kabla ya kumkata jamaa aliyekuwa akisafirisha mzigo huo kwa pikipiki.

Afisa huyo anasema kwa sasa wanaendelea na uchunguzi kubaini mmiliki wa mzigo huo huku wakiendelea kumzuia mwendeshaji wa pikipiki aliyekuwa anausafirisha katika  barabara kuu ya Malindi-Lamu

Kwa upande mwengine,Kemboi ametoa onyo kwa waraibu pamoja na walanguzi akisema maafisa wake wako macho kuwatia mbaroni na kuwafungulia mashta.

Kemboi amesisitiza kuwa idara ya upelelezi pamoja na vitengo vya usalama havitasita kuwakamata walanguzi wote wa mihadarati eneo hilo.