HabariLifestyleNews

SEKTA YA UTALII YAMPONGEZA GAVANA JOHO KWA KUPUNGUZA ADA…..

Washikadau katika sekta ya utalii hapa mjini mombasa  wameipongeza hatua ya gavana wa mombasa Hassan Joho kuondoa na pia kupunguza baadhi ya ada wanazo tozwa na serkali ya kaunti hiyo.

Hii ni kutokana na hali ngumu ya kiuchumi inayoikumba sekta  tofauti za utalii katika kaunti hiyo  na kumfanya Gavana Joho kuchukua hatua hadi uchumi utakapoimariika.

Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa Joho amesema ni wazi kuwa sekta ya utalii inaotegemewa pakubwa Mombasa imeathirika na janga la Corona ivyo ipo haja ya kuwapunguzia ada na pia kuwapa muda zaidi kulipia baadhi ya leseni zao.

Gavana Joho ameongeza kuwa wale ambao hawana uwezo wa kutoa malipo yote kwa wakati mmoja wanaruhusiwa kulipa kidogo kidogo kulingana na mpango utakao tolewa na kitengo cha fedha.

By News Desk