AfyaHabari

WANAOISHI NI VIRUSI VYA UKIMWI KWALE WAONDOLEWA HOFU KUFUATIA UHABA WA DAWA………….

Serikali ya kaunti ya Kwale imewataka wagonjwa wa virusi vya ukimwi kaunti hiyo kuondoa hofu kufuatia uhaba wa dawa za kukabili makal ya ugonjwa huo humu nchini

Waziri wa afya kaunti hiyo Francis Gwama amesema kuwa kuna dawa za kutosha za kuwasaidia wagonjwa hao kwa muda miezi miwili.

Aidha amesema wanatarajia kupokea dawa hizo zinazotolewa bila malipo yoyote kutoka wa serikali ya kitaifa hivi karibuni

Zaidi ya wagonjwa 2000 wanategemea dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi