Habari

KPLC yakumbwa na hitilafu katika mfumo wake wa kununua tokens…

Kampuni ya kusambaza nguvu za umeme ya KPLC imeeleza kukumbwa na hitilafu katika zoezi la kununua mjazo wa umeme maarufu TOKEN kwa wateja wake kuanzia jana.

hii ni baada ya baadhi ya wakenya kukaa bila umeme baada ya mfumo wa kununua mjazo huo wa umeme kukumbwa na hitilafu.

KPLC hii leo kwenye taarifa yake inasema imefanikiwa kutatua tatizo hilo la kimitambo lakini ikasema zoezi la kununua mjazo huo bado liko pole pole.

Inasema kwa sasa inashughulikia tatizo hilo ili kuhakikisha ununuzi wa tokens unaregea katika hali ya kawaida katika sehemu zote zile za ununuzi.

ikumbukwe kuwa mwezi mmoja uliopita, waziri wa kawi Charles Keter na mkurugenzi mkuu wa KPLC Bernard Ngugi walitakiwa kufika mbele ya maseneta kufuatia kupotea kwa umeme kila mara humu nchini.

By Warda Ahmed