Habari

Majaji 3 waskiza rufaa ya JSC kuhusu wanaotafuta nafasi ya jaji mkuu….

Jaji Rosylne Nambuye anaongoza kikao cha majaji watatu wanaosikiza rufaa iliyowasilishwa na tume ya huduma za mahakama JSC kuhusiana na kuwahoji wanaotafuta kujaza nafasi ya jaji mkuu.

Majaji wengine wanaosikiza kesi hiyo ni pamoja na jaji Patrick Kiage, na Sankale Ole Kantai.

JSC iliwasilisha rufaa baada ya majaji Anthony Mrima, Robin Nyakundi na Wilfrida Okwan kusitisha kutolewa kwa uamuzi huo kuhusu nani atayekuwa jaji mkuu na pia msasa wa wanaotaka kuwa jaji wa mahakama ya juu.

Kikao hicho kinaendelea kwa sasa.

Na Warda Ahmed