AfyaHabariNews

Hospitali kuu mjini Malindi yaweka mikakati ya kudhibito corona…….

Hospitali kuu mjini Malindi kaunti ya Kilifi imeweka mikakati kabambe ya kuthibiti maambukizi ya virusi vya Corona Hospitalini humo.

 

Kulingana na msimamizi mkuu wa Hospitali hiyo Daktari  Job Gayo, kwa sasa hispitali hiyo inaruhusu watu wanne pekee kuangalia mgonjwa kwa nyakati tofauti.

 

Kwenye mahojiano ya kipekee na kituo hiki Gayo amesema hatua hiyo inalenga kupunguza msongamano wa watu katika Hospitali hiyo ili kutowahatarisha wagonjwa dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

 

 

Wakati uohuo msimamizi huyo amebainisha kuwa tayari hospitali hiyo imeripoti visa vya wagonjwa walioambukizwa virusi vya corona katika Hospitali hiyo licha ya kutoonyesha dalili za kuugua virusi hivyo.

 

Aidha amesisitiza haja ya wanaoingia katika wodi za Hospitali hiyo kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya ya kuthibiti msambao wa Corona.

 

By Malindi Correspondent Joseph Yeri