BurudaniEntertainment

MJUE MSANII WAKO [MORENO KEVIN] PRINCE LUCKY.

Moreno Kevin kwa jina la kimajazi Prince Lucky ni msanii chipukizi wa mziki wa aina Afro pop na Afro fusion kutoka Kenya. Alizaliwa mjini Kisii na kisha baadaye kugura na kwenda jijini Nairobi. Azma ya kufanya mziki ilimjaa na akaanza kujituma akiwa bado mchanga ambapo alikuwa akikariri mashairi katika tamasha za mziki na drama na alipenda sana kuimba.

Alianza kuimba katika mainstream mwaka 2018 alipoachilia kibao kwa jina ‘Mahabuba’ ambacho kilimjuza rasmi kwenye industry na baadae kutoa kazi nyinginezo. Mwaka 2020 alisigniwa ndani ya Vinnox Records Label ilioko jijini Nairobi ambapo kwa sasa anatoa nyimbo baada ya nyimbo.

Kazi nyingine ambazo amefanya ni kama vile; Tutafika, African Queen, Acha ikae, Fire. Na mpate katika mtandao wa facebook kama Prince Lucky¬† na page yake kama Official’prince Lucky, Instagram anapatikana kama official princelucky upande wa twitter ni Princelucky_254 na youtube ni Prince Lucky.

By Leon Nkaduda