Huku ulimwengu mzima ukiadhimisha siku ya uhuru ya vyombo vya habari hii leo, hisia tofauti zimetolewa na baadhi ya wanahabari pamoja na wakenya wakidai kuwa bado vyombo vya habari nchini havijapewa uhuru ikilinganishwa na katiba.
Meneja wa kituo cha habari cha Sauti ya Pwani Sammy Mwaura,anasema kuwa siku hii ya leo ni siku ya maana hasa katika maisha ya waandishi wa habari licha ya changamoto wanazozipitia wanapokuwa katika harakati za kufanya majukumu yao.
Hata hivyo mwaura anaeleza kuwa uhuru vya vyombo vya habari nchini bado haujapewa kipao mbele kama inavyodaiwa kikatiba.
Kwa upande wake mhariri mkuu katika kitengo cha habari hapa sauti ya Pwani Warda Ahmed ,anahofia maisha ya waandishi wa habari akidai kuwa usalama wao uko hatarini wanapofanya kazi zao haswa wale wanaofanya habari za uchunguzi.
Mkuu wa kitengo cha michezo JK Makaniki vile vile anahisi kwamba vyombo vya habari bado havina uhuru kama inavyodaiwa.
Kwa upande wake mratibu wa baraza la wanahabari nchini MCK kanda ya Pwani Maureen Mudi amewahimiza wanahabari kuhakikisha kwamba wanaripoti visa vyovyote vinavyohujumu kazi zao kwa baraza hilo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Information as a public good.
Siku ya uhuru wa wanahabari huadhimishwa kila tarehe 3 ya mwezi mei.
By Reporter David Otieno.