Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amevionya vyombo vya habari na watumiaji wa mitandao ya kijamii dhidi ya kuchochea wasiwasi kwa wakenya juu ya kutolewa kwa matokeo ya KCSE.
Akizungumza katika shule ya upili ya Wavulana ya Starehe jijini Nairobi baada ya kukamilika rasmi kwa usahihishaji wa mtihani wa kidato cha nne KCSE, Magoha amesema wizara yake itatoa mwelekeo wakati matokeo ya mtihani yatakapokuwa tayari.
Aidha Magoha ameongezea kwamba shule zitafunguliwa jumatatu juma lijajo kama ilivyoratibiwa, akiongeza kuwa serikali iko mstari wa mbele kuona kuwa walimu wote wanapokea chanjo ya Corona kufikia mwisho wa mwezi ujao
Haya yanajiri huku fununu zikisambaa mitandaoni kwamba matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yalitazamiwa kutolewa hii leo.
By Nicky Waita