Akizungumza na meza yetu ya habari mkurugenzi mkuu wa chuo hicho Daktari Wilfred Githinji aliyekuwa akiongoza shughli ya kutoa iftar iliyowahusisha waislamu na wakristo katika Chuo kikuu cha Kemu hapa jijini Mombasa, Githinji amesema shughli hiyo ni njia moja wapo ya kujenga uhusiano mwema baina yao.
Aidha githinji amesisitiza kuwa kulingana na mapokezi walipata baada ya kutoa iftur hiyo kwa sasa wanalenga kuzidi kutoa ili kuimairisha uhusiano huo.
Kwa upande wake Imam Ali Abdin wa msikiti lutar amepongeza hatua hiyo akidai kuwa hilo ni jambo la kupigiwa mfano
By David Otieno