Habari

Kuna haja ya kuzileta pamoja dini ya kislamu ya ile ya kikristo ili waziidi kushirikiana na hata kujenga amani baina yao…..

Akizungumza na meza yetu ya habari mkurugenzi mkuu wa chuo hicho Daktari Wilfred Githinji aliyekuwa akiongoza shughli ya kutoa iftar  iliyowahusisha waislamu na wakristo katika Chuo kikuu cha Kemu hapa jijini Mombasa, Githinji amesema shughli hiyo ni  njia moja wapo ya kujenga uhusiano mwema baina yao.

Aidha githinji amesisitiza kuwa kulingana na mapokezi walipata baada ya kutoa  iftur hiyo kwa sasa wanalenga kuzidi kutoa ili kuimairisha uhusiano huo.

Kwa upande wake Imam Ali Abdin wa msikiti lutar amepongeza hatua hiyo akidai kuwa hilo ni  jambo la kupigiwa mfano

 

By David Otieno