Chama cha kutetea walimu nchini KNUT tawi la pwani kimetoa wito kwa serikali kupitia wizara ya elimu na fedha kutoa fedha za kugharamia elimu ya bure mapema wakati huu ambapo shule tayari zimeanza kufunguliwa.
Akizungumza na meza yetu ya habari katibu wa chama hicho tawi la kilindini Mwalimu Dan Aloo, amesema kuwa licha ya walimu kuwa tayari katika ufunguzi wa shule ni sharti seriklai iweze kutuma fedha hizo mapema ili shughuli za masomo ziweze kuendelea bila shida yoyote.
Aidha ametoa wito kwa tume ya kuajiri walimu nchini TSC kuongeza idadi ya walimu katika shule mbali mbali nchini vile vile kuwapandisha vyeo walimu waoitimu ili kuboresha sekta hiyo, kadhalka ametaka walimu kufanya kazi kwa pamoja katika kufanyikisha ajenda ya masomo nchini.
By News Desk