HabariNews

Wavuvi Lamu hawana imani na zoezi la usajili wa watakaopokea fidia…

Jamii ya wavuvi eneo la kiunga kaunti ya Lamu wanasema hawana imani na  zoezi la kusajili majina ya wavuvi ambao watapokea malipo kutokana na kufungwa kwa maeneo yao ya kuvulia samaki. Wavuvi hawa wanasema zoezi hili linakumbwa na udanganyifu mkubwa, wakisema majina ambayo saa hii yamesajiliwa mengi si ya wavuvi.

Sasa wavuvi hawa wametaka serikali kushirikiana na wavuvi wenyewe katika usajili wa majina hayo ili kuhakikisha fedha hizo zinawafaidi walengwa.

Hatua ya kuwalipa wavuvi inakuja baada ya jamii hiyo kulalamikia kuharibiwa kwa sehemu zao za kuvulia samaki kufatia shughuli ya ujenzi wa bandari ya Lamu.

By Guracho Salad