Habari

Shule ya wavulana ya Kilifi Township yaandikisha matokeo bora katika mtihani wa KCSE…….

Shule ya upili ya wavulana ya Kilifi Township katika eneo bunge la Kilifi Kaskazini inadaiwa kuandikisha matokeo bora katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE mwaka wa 2020.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Charo Katana, shule hiyo imeandikisha matokeo bora ya mtihani wa KCSE ikilinganishwa na miaka ya hapo nyuma.
Charo amesema wanafunzi 138 ambao walifanya mtihani huo wengi wao walifanikiwa kupata alama zinazowawezesha kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali nchini, huku akiongeza kuwa somo la kilimo ndilo limeandikisha matokeo bora zaidi shuleni humo.

Kwa upande wake mwalimu wa somo la kilimo Manfred Muga amesema ushirikiano wake na wanafunzi ndio uliwawezesha kuandikisha matokeo bora zaidi.
Hata hivyo amewataka wanafunzi wengi kufanya masomo ya ukulima ili waweze kupata mbinu za kujijenga katika kilimo biashara baada ya masomo ya kidato cha nne.

By Kilifi Correspondent Erickson Kadzeha.