Habari

Wakaazi wa SABAKI Magarini walalamikia huduma duni za utoaji wa neti……..

Baadhi ya wakaazi wa Sabaki eneo bunge la Magarini Kaunti ya Kilifi wanalalamikia huduma duni kwenye zahanati ya Mijikenda haswa katika ugavi wa vyandarua vya kuzuia mbu eneo hilo.

Wakiongozwa na Shilla Athman na Elizabeth Japheth wanadai kwamba hata baada ya kuandikishwa kupitia wazee wa nyumba kumi kupata vyandarua hivyo, idadi kubwa ya wakaazi hao bado hawajapokea neti hizo.

Waziri wa afya kaunti ya Kilifi Charles Dadu amethibitiha kupokea baadhi ya malalamishi kutoka kwa wakaazi wa Kilifi huku akisema kwamba wahusika watakabiliwa kwa mujibu wa sheria punde ripoti kamili itawasilishwa na maafisa wa nyanjani baada ya kubaini wale waliokosa neti hizo katika kaunti ya Kilifi.

By Reporter Nick Waita