HabariSiasa

Wakili tajika George Kithi amekashifu vikali kauli ya seneta wa migori Ochilo Ayako…

Wakili tajika ambaye pia ni mwaniaji wa kiti cha useneta kaunti ya kilifi George Kithi amekashifu vikali kauli ya seneta wa migori Ochilo Ayako ya  kwamba mahakama ya juu ilikiuka sheria ilipokuwa ikiamuru kuwa BBI ni ripoti gushi

Kithi amesema kuwa hakuna vile ripoti hiyo inaweza kushinda kesi katika Mahakama ya rufaa kutokana  na vipenge vingi ambavyo vilikiuka sheria wakati  ambapo mswada huo ulikuwa unaundwa, kauli ambayo kwa upande wake Ayako ambaye pia ni wakili anasema inawezekana kwani rais ni mkenya na ana uwezo wa kusukuma mswada wa kubadilisha katiba kulingana na kipengee cha 257.

Kithi amesema haya katika mahojiano ya kipekee kwenye kipindi cha baraza letu hii leo siku chache baada ya ripoti kubatilishwa na mahakama ya juu kwa kukoosa kuzingatia katiba.

Wakati huohuo kiongozi wa  vugu vugu la United For Green Movement ambaye pia ni mwaniaji wa kiti cha wawakilishi wa kike kaunti ya mombasa Khamisa Zaja ametoa pongezi kwa jopo la majaji watano walioamuru ripoti ya BBl meundwa kinyume cha sheria.

Katika mahojiano ya kipekee na Sauti Ya Pwani Zaja amesema kuwa ripoti hiyo ilikuwa inaenda kuwagawanya wakenya kwa misingi ya kikabila pasi na kuleta wakenya  Pamoja.

Zaja ni miongoni mwa viongozi wa ukanda wa Pwani walioanza mchakato wa kupinga ripoti hiyo mapema punde tu ilipoundwa.

Kwa sasa Zaja amewasihi viongozi kurudi kuchukua fursa hiyo kuanza mikakati ya kuanzisha miradi ya kuboresha kenya kupitia ajenda nne kuu zilizoachwa na mpatanishi wa amani Kofi Annan badala ya kupoteza rasilimali katika mchakato huo.

BY DAVID OTIENO