HabariNews

Wafanyibiashara wa soko la Showground huko Ukunda kaunti ya Kwale wakadiria hasara…

Wafanyibiashara wa soko la Showground huko Ukunda kaunti ya Kwale wanakadiria hasara ya bidhaa zao baada ya kukosa wateja katika sikukuu ya Eid.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Peter Mutugi, wanasema kuwa idadi ndogo ya wateja imejitokeza katika soko hilo wakati wa kuidhimisha sikukuu hiyo kwa waislamu.

Wafanyibiashara hao wameeleza kuwa matumaini ya kuimarika kwa biashara zao yamedidimizwa baada ya bidhaa zao kuharibikia sokoni.

Kutokana na hali hiyo sasa, wafanyibiashara hao wanaitaka serikali ya kaunti ya Kwale kuwapatia mikopo ya kujiendeleza kibiashara.

Wanadai kupitia changamoto nyingi za kimaisha huku baadhi yao wakidaiwa mikopo waliyochukua baada ya biashara zao kuathirika na janga la corona

BY BINTIKHAMIS MOHAMMED