HabariMombasaSiasa

Mbunge wa Mvita awatahadharisha wananchi na wanasiasa wa dakika za mwisho….

Mbunge wa mvita Abdulswamad Shariff Nassir amewatahadharisha wananchi dhidi ya wanasiasa wanaoibuka nyakati za uchaguzi unapokaribia wakiahidi maendeleo  mashinani huku akiwaita kama manabii waongo.

Akizungumza na wakaazi huko Junda Mlango Saba eneo bunge la Kisauni Abdulswamad amesema ni wakati sasa kwa wananchi kuwa macho kwani kunapokaribia uchaguzi mkuu wanasiasa wengi hujitokeza wakifanya wanyenyekevu.

Abdulswamad ametaja hali hio ya viongozi kama ubinafsi wa kimaslahi kwani wengi wakipata walichokililia hawajali wananchi walioko mashinani.

By Reporter