HabariSiasa

Bunge la kitaifa kesho kujadili uteuzi wa Martha Koome kwa wadhfa wa jaji mkuu…

Bunge la kitaifa hapo kesho linatarajiwa kujadili ripoti ya kamati ya haki na masuala ya sheria kuhusu uteuzi wa Martha Koome kujaza wadhfa wa jaji mkuu nchini.

Spika wa bunge hilo Justin Muturi tayari amechapisha kwenye gazeti rasmi la serikali kutengwa kwa muda kuijadili ripoti hiyo baada ya Koome kuchujwa na kamati hiyo siku ya alhamisi iliyopita.

Koome ambaye ana uzoefu wa kazi ya uanasheria kwa zaidi ya miaka 30 anapigiwa upatu na wengi na huenda akatwaa wadhfa huo ambao uliachwa wazi kufuatia kustaafu kwa mtangulizi wake DAVID Maraga.

By Reporter Warda Ahmed