HabariSiasa

Hatua ya kumbandua gavana wa Wajir mamlakani yachapishwa kwenye gazeti la serikali…….

Spika wa bunge la seneti Ken Lusaka amechapisha rasmi kubanduliwa kwa Mohamed Abdi kama gavana wa Wajir katika gazeti rasmi la serikali kufuatia madai ya ufisadi na utumizi mbaya wa afisi.

Lusaka amechapisha mchakato mzima wa kisheria ulioafikia hatua ya kumbandua mamlakani.

Haya yanajiri huku maandalizi ya kuapishwa kwa naibu gavana wa kaunti ya Wajir Ahmed Ali Muktar kuwa gavana yakiendelea kwa sasa na ataapishwa muda wowote kuanzia sasa ambapo atahudumu kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja na nusu kilichosalia.

Hata hivyo wakaazi wa Wajir wametoa hisia mseto kuhusu hatua ya bunge la seneti kumbandua gavana Mohamed Abdi Mohamud.

Jumla ya maseneta 25 walipiga kura ya kuidhinisha ripoti ya kamati iliyokuwa ikichunguza madai ya ufisadi, utumizi mbaya wa mamlaka yaliyoibuliwa na wawakilishi wadi wa kaunti ya Wajir dhidi ya gavana huyo.

By reporter Warda Ahmed