HabariSiasa

VIJANA UKANDA WA PWANI WAHIMIZWA KUWEKEZA KAUNTI YA LAMU.

Siku chache tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kufungua rasmi bandari ya Lamu, vijana ukanda wa Pwani wamehimizwa kuwekeza katika kaunti hiyo.

Akizungumza mjini Kilifi mkurugenzi mkuu  wa ruwaza ya mwaka wa 2030 nchini Kenneth Mwige, amesema kufunguliwa kwa bandari ya Lamu kunatoa nafasi za biashara  na kuwataka vijana eneo la Pwani kutumia fursa hiyo kujiendeleza.

Aidha ameongeza kuwa changamoto ya uhaba wa nafasi za kufanyia biashara imeanza kushuhudiwa Lamu.

Migwe ameeleza kuwa njia rahisi kwa vijana kunufaika ni kwa kujiunga makundi na kuomba mikopo ili waweze kufanya biashara eneo hilo.

Amesema serikali inajizatiti kuimarisha uchumi kupitia miradi mbali mbali ambayo itabadilisha maisha wa wananchi ufikapo mwaka wa 2030.

 

BY ERICKSON KADZEHA