HabariSiasa

Jaji Martha Koome akabidhiwa rasmi mamlaka ya kuwa jaji mkuu

Jaji mkuu Martha Koome amekabidhiwa rasmi mamlaka ya kuwa jaji mkuu wa kwanza mwanamke humu nchini na rais wa mahakama ya juu.

Shughuli hiyo imefanyika katika mahakama ya juu, na kuongozwa na msajili wa idara ya mahakama Ann Amadi na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa serikalini.

Naibu Jaji mkuu Philomena MWILU amemkabidhi rasmi afisi hiyo na zana za kazi.

Jaji Koome aliapishwa ijumaa iliyopita na kuwa jaji mkuu wa tatu humu nchini chini ya katiba ya sasa, katika hafla iliyohudhuriwa na rais Uhuru Kenyatta katika ikulu ya Nairobi.

Katika hafla hiyo jaji William Ouko pia aliapishwa kuwa jaji wa mahakama ya juu , huku wote wawili wakiahidi kutetea katiba ya nchi na kulinda uhuru wa idara ya mahakama.

 

By Warda Ahmed