Habari

Makafani ya hospitali ya Kilifi kufunguliwa mwezi ujao…….

Makafani katika hospitali ya rufaa kaunti ya Kilifi  yanatarajiwa kufunguliwa rasmi mwezi juni.

Kulingana na waziri wa afya kaunti ya Kilifi Charles Dadu, makafani hayo yaliyofungwa tangu mwezi Machi yanatarajiwa kurejelea shughuli zake za kawaida pindi eneo la kuegesha magari na mahali pa watu kufanyia maombi miili ya wapendwa wao wanapoitoa pakimalizika kujengwa.
Amesema makafani ya sasa yanauwezo wa kuhifadhi miili 40 pamoja na uwezo wa kufanyia upasuaji wa miili mitatu kwa wakati mmoja.

Kwa upande wao wafanyabiashara ya majeneza wamelalamikia hatua ya kucheleweshwa kwa kufunguliwa rasmi makafani hiyo, huku wakiongeza kuwa biashara zao zinaendelea kufilisika.

Makafani katika hospitali hiyo ya rufaa yalifungwa ili kutoa nafasi ya kuhamisha vifaa hadi kwenye makafani mpya, shughuli iliyotarajiwa kuchukua muda wa wiki mbili.

By Kilifi correspondent