HabariSiasa

WAZIRI WA LEBA SIMON CHELUGUI AZURU TAASISI YA KIUFUNDI KATIKA KAUNTI YA MOMBASA

Waziri wa leba Simon Chelugui anazuru taasisi ya kiufundi katika kaunti ya Mombasa kutathmini mikakati ya kukuza viwango vya wanaojiunga na taasisi hizo pamoja na kujitaftia ajira baada ya kukamilisha mafunzo.

Ziara hiyo pia inalenga kukagua miradi mbalimbali ya serikali ili kuboresha utendakazi.

Waziri Chelugui amesema kuwa mtihani unaendelea katika vyuo vya kiufundi  nchini, huku watahiniwa zaidi ya 30,000 wakikalia mtihani huo.

Chelugui ameongeza kuwa umuhimu vyuo vya kiufundi nchini ni kuwapa vijana  taaluma mbalimbali ambazo zitawasaidia kuajiriwa na hata kujiari wenyewe.

Hata hivyo watahaniwa kaunti ya Samburu hawatafanya mtihani huo kutokana na janga la Corona.

 

BY JOYCE MWENDWA