Habari

SERIKALI YA KAUNTI WYA TAITA TAVETA YAKAMILISHA MAFUNZO MAALUM YA ZIMA MOTO…..

Serikali ya kaunti ya Taita Taveta kupitia idara ya kazi za umma uchukuzi na muindo mbinu imefaulu kukamilisha mafunzo maalum chini ya wiki moja wa kikosi cha zima moto kaunti hiyo.

haya yanajiri mwezi moja tu baada ya kaunti hiyo kununua magari ya kuzima moto kutokana na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wafanyibiashara hasa mjini voi.

hatua hii ikiwa ni mwamko mpya kwa wafanyibiashara katika kaunti hiyo na pia kwa waekezji huku ikitoa hofu ya ukosefu wa vifaa vya kuzima moto iwapo visa hivyo vitaripotiwa

afisa mkuu wa zima moto kaunti ya Kilifi Saul Kahindi ameutaja ujio wa magari hayo kama afueni kwao kwani wamekuwa wakiitwa mara kwa mara kusaidia kaunti ya taita taveta kukabiliana na mikasa ya moto

Kulingana na waziri wa ujenzi na uchukuzi kaunti hiyo Gasper Kahindi ameitaka kaunti hiyo kufungua akaunti ya kaunti hiyo katika mtandoa wa facebook ili iwasaidie katika mawasiliano.

BY JOYCE MWENDWA