HabariMombasa

Waakazi Kibarani wataka kupewa ajira katika ujenzi wa daraja eneo hilo…………….

Wakaazi eneo la Kibarani hapa Mombasa wametoa malalamishi yao wakitaka kupewa nafasi za ajira katika mradi wa ujezi wa daraja la kibarani,daraja linalounganisha eneo la changamwe na kisiwa cha Mombasa.

Wenyeji  hao wameyasema haya kwa misingi kuwa tangu ujenzi huo uanze rasmi hakuna hata mkaazi mmoja katika eneo hilo amepata ajira.

Hata hivyo wito wao ni kwa viongozi wakuu serikalini kumuamuru mwanakandarasi huyo kuwakumbuka wakaazi hao hata kwa kazi za vibarua.

 

By Reporter Gladys Marura