HabariMombasaSiasa

Hatua ya rais kuvunja utaratibu katika sherehe za madaraka yakosolewa vikali……..

Mkeretwa wa masuala ya usalama na siasa ambae pia aliwania kiti cha ubunge katika eneo bunge la Changamwe Abdi Daib amekashifu vikali hatua ya hapo jana ya kuvunja taratibu katika sherehe ya madaraka kwa kumhurusu kinara wa ODM raila Odinga kuzungumza baada ya naibu wa rais Wilium Ruto.

Akizungumza katika kipindi cha sauti asubuhi hii leo  Daib amesema kuwa rais alifanya hivyo kufurahisha jamii kutoka Kisumu pasi na kujali sheria jambo ambalo ni kinyume cha sheria na kumkosea heshima naibu wake.

Kadhalika daib ameongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona kwamba rais kenyatta kutaka kuonesha idara ya Mahakama jinsi ya kufanya kazi kwani kulingana na katiba kila idara ina jukumu lake la kufanya pasi na kuingiliwa na mwingine.

 

By David Otieno