HabariMazingira

Wanakandarasi wanaokarabati barabara Tanariver watakiwa kuwajibika……..

Wanakandarasi wanaotekeleza ujenzi na ukarabati wa barabara za mashinani kaunti ya TanaRiver wametakiwa kuwajibika na kutekeleza majukumu yao kwa ubora wa hali ya juu kama ilivyonakiliwa kwenye stakabadhi za kandarasi.

Mwenyekiti wa kamati za barabara katika bunge la kaunti hiyo Salim Bonaya amesema wamepanga ratiba ya kutembelea barabara ambazo ujenzi unaendelea ili kukagua na kutathmini utendakazi.

Bonaya amewataka wanakandarasi wasiangazie maswala ya kupata pesa katika utekelezwaji wa miradi bali wazingatie swala la huduma kwa wananchi.

 

By Joyce Mwendwa