HabariMombasa

Idara ya Upelelezi Kushirikiana na viongozi wa Kidini ili Kuimarisha Usalama Likoni………………………

Afisa mkuu wa kitengo cha upelelezi wa jinai katika gatuzi dogo la Likoni Richard K`oywer amesema kwamba watashirikiana na muungano wa viongozi wa kidini CICC katika  harakati za kupambana na utovu wa usalama katika maeneo tofauti ya hapa Mombasa haswa wakati huu tunaoelekea uchaguzi mkuu.

Akizungumza kwenye kongamano lililowaleta pamoja viongozi hao wa kidini pamoja na vitengo vya usalama kutoka maeneo ya Likoni na Changamwe hapa Mombasa, K`oywer amedokeza  kwamba idara yake ina mbinu tofauti ya kupata habari muhimu za utovu wa usalama.

Kwa upande wao viongozi hao wa Imani tofauti wamelezea kufanya vikao vya mara kwa mara na vitengo vya usalama pamoja na wazazi katika maeneo wanamoishi ili kutoa ripoti ya usalama kwenye maeneo yao ili kukabili utovu wa usalama unaoshuhudiwa hususan wakati wa uchaguzi mkuu.