Habari

Familia zinazojiweza zatakiwa kulipa karo kwa wakati ufaao……

Waziri wa elimu profesa George Magoha amewaamuru wakuu wa shule kote nchini kuhakikisha kwamba wanafunzi wote ambao wametoka katika familia ambazo zinauwezo,  kulipa karo ya muhula wa tatu bila kuchelewa.

Aidha Magoha pia amewataka wakuu hao kuangazia swala la kutowatuma nyumbani wanafunzi wasio na uwezo wa kulipa karo kutokana na changamoto ya wazazi wao kukosa ajira kutokana na janga la Corona.

Haya yanajiri huku  Serikali tayari ikituma mgao wa fedha utakaogaramia shughuli za masomo kwa shule zote za umma hapa nchini huku shughuli za masomo zikirejea tena hii leo baada ya likizo fupi iliochukua siku tatu.

Kulingana na waziri wa elimu profesa George Magoha, shilingi billioni 9.3 zimetolewa kwa shule za msingi na zile za upili.

Shule za msingi zitapokea mgao wa fedha wa shilingi bilioni 2.8 huku shule za upili zikigawiwa shilingi bilioni 6.5.

Shule hizo zitafugwa kwa takriban wiki mbili mwezi ujao kabla ya kuanzwa kwa muhula ujao.

 

By Nicky Waita