Habari

Ulanguzi wa watoto wachipuka kaunti ya Kwale…….

Visa vya ulanguzi wa watoto vimeanza kuchipuka kaunti ya Kwale kufuatia utumizi mbaya wa mitandao ya kijamii miongoni mwa watoto wadogo wanaodhulumiwa kimapenzi.

Haya ni kwa mujibu wa mwanaharakati wa kutetea haki za watoto kaunti hiyo Harun Omariba anayesema kwamba hali hiyo imechangiwa na janga la corona.

Kwenye mahojiano ya kipekee, Omariba amesema kuwa hatua hiyo imechangia visa vya watoto wanaopotea kiholela kuongezeka nchini.

Mwanaharakati huyo sasa anawataka wazazi kaunti hiyo kuwaelimisha watoto wao kama njia mojawapo ya kukabiliana na visa vya dhulma.

Omariba aidha amewataka wazazi kuwa karibu na wanao ili kuwaepusha na visa vya ulanguzi vinavyotekelezwa kupitia mitandao ya kijamii.

 

By Kwale Correspondent