Habari

Nyumba za baadhi ya wakaazi MTWAPA yateketezwa……

Makaazi ya baadhi ya wakaazi eneo la Mtwapa kaunti ya Kilifi yameteketezwa na watu wasiojulikana kufuatia mgogoro wa ardhi yenye ekari 72.

Wakaazi hao wanaitaka serikali isuluhishe mzozo ardhi hiyo wakilalamikia kuhangaishwa mara kwa mara na watu wanaodai kuimiliki ardhi hiyo.

Haya yanajiri licha ya Mahakama mjini malindi kutoa uamuzi kuhusu kesi ya ardhi hiyo, wakaazi hao wakidai haukuwa wa haki hivi basi wakimtaka jaji mkuu kuingilia kati

 

By Joyce Kelly