Habari

SERIKALI YATENGA BILIONI 142.1 KUENDELEZA AJENDA NNE KUU ZA MAENDELEO………………….

Makadirio ya bajeti ya mwaka wa kifedha 2021/2022 ambayo ni shilingi trilioni3.6 imesoma hii leo na Waziri wa Fedha Ukur Yattani katika bunge la kitaifa.

Yattani amesema serikali imetenga shilingi bilioni 142.1 kuendeleza ajenda zake nne kuu za maendeleo ili kubuni nafasi zaidi za ajira ya 100,000 baada ya kufanikisha miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa bandari ya Lamu, reli ya kisasa ya SGR, ufufuzi wa kiwanda cha nguo cha rivertex mjini Eldoret na ufufuzi wa kiwanda cha nyama KMC

Serikali imetenga shilingi bilioni 14.3 ili kufanikisha mpango wa kuwachanja wakenya dhidi ya virusi vya Corona huku shilingi bilioni 8.7 zikitengewa dharura ya wagonjwa wa Covid 19.

Aidha shilingi bilioni 1.2 zimetengwa kwa ajili ya uwajiri wa wahudumu wa afya huku shilingi bilioni 121.1 katika kuhakikisha huduma bora za afya kwa wote UHC unakamilika.

Vilevile shilingi bilioni 4.1 zimetengwa kuboresha huduma katika vituo vya afya vya akina mama kuhakikisha wamama hawafariki wanapojifungua.

BY JOYCE MWENDWA