HabariMombasa

SENETA FAKI AMLAUMU RAIS UHURU KENYATTA

Senata wa mombasa Mohammed Mwinyi Faki anazidi kumlaumu rais Uhuru Kenyatta akisema kuwa anaongoza taifa kwa njia isiyofaa baada ya kushindwa kuheshimu katiba ya taifa kwa kutowateuwa majaji 6 licha ya majina yao kuwasilisha na tume ya huduma za mahakama JSC.

Akizungumza na wandishi wa habari mjini Mombasa, Faki amesema kuwa kulingana na sheria rais wa jamhuri ya kenya hawezi kusita kuwateuwa majaji waliopendekezwa na tume ya JSC huku akimshauri kuwateuwa na kisha kuwasilisha malalamishi yake mbele ya tume hiyo.

Wakati huo huo Faki amewaunga mkono baadhi ya wabunge kutoka ukanda wa Pwani kwa kile wanachokidai kubaguliwa katika zoezi la kuchukua maafisa wa misitu iliyokamilika siku chache zilizopita.

 

By David Otieno