AfyaHabari

Maambukizi ya HIV kwa waathiriwa wa mihadarati yapungua……

Afisa katika kituo cha kurekebisha tabia MEWA hasa kwa watumizi wa mihadarati Hussein Abdallah amesema kuwa kwa sassa kituo hicho kimefaulu kupunguza maambukizi ya virusi vya HIV kwa waathariwa wa  dawa za kulevya.

Akizungumza katika kipindi cha sauti asubuhi Abdallah amesema kupita mfumu huo wa kuwarekebisha  tabia waathiriwa ambao wanaamika kuambukizwa maradhi mbali mbali ikiwemo virusi vya HIV idadi kubwa ya waathiriwa wamepata afueni huku idadi ya maambukizi hayo yakipungua kwa kiwango kikubwa.

Wakati huo huo Hussein ametoa wito kwa serikali kupitia rais uhuru kenyatta kutotia saini mswada kuhusu midarati uliowasilishwa mbele yake kabla kusoma na kuuelewa zaidi kwani mswada huo ulipitishwa na wabunge bila kuangazia maslahi muhimu.

Kadhalka ameongeza kuwa serikali inapaswa kutilia mkazo sheria iliyoundwa mwaka wa 1994 kudhibiti matumizi ya mihadarati hasa kipenge kinacho waruhusu waathiriwa kupelekwa katika vituo vya kubadili tabia mbali na kuwakamata na kuwafunga.

 

By David Otieno