HabariSiasa

Viongozi wa kisiasa Kilifi wametakiwa kudumisha umoja……

Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Kilifi wametakiwa kudumisha umoja kwa manufaa ya mkaazi wa kaunti hiyo.

Katika mahojiano ya kipekee, mwakilishi wadi ya Mwanamwinga Pascal Makanga amesema kuwa kumekuwa na minung’uniko mingi baada ya wawakilishi wadi kufanya mkutano na mbunge wa Malindi Aisha Jumwa kujadili kuhusu azma yake ya kuwania ugavana mwaka ujao.

Makanga amedokeza kuwa huu si wakati wakujadii mirengo bali viongozi wanafaa kujadili mstakabali wa maendeleo na Jumwa alikua na haki kama kiongozi wa Kilifi kufanya mazungumzo na wawakilishi wadi yeye akiwa miongoni mwao.

Kuhusiana na maswala ya elimu Makanga amekinzana na agizo la waziri wa elimu prof George Magoha la kuwataka wazazi kumalizia kulipa karo za watoto wao kabla ya muhula wa kwanza kuanza rasmi mwezi ujao akisema kuwa agizo hilo huenda likaathiri elimu ya baadhi ya wanafunzi.

 

By Correspondent