HabariNews

Vijana wahusishwe katika vita dhidi ya dhulma za kijinsia………

Mashirika ya kijamii yameshauriwa kuwahusisha vijana katika vita dhidi ya dhulma za kijinsia katika kaunti ya Kwale ili kupunguza ongezeko la visa hivyo,hii ni baada ya kubainika kuwa waendeshaji bodaboda kaunti hiyo huhusika pakubwa katika visa vya kuwapachika wanafunzi mimba na kuwaingiza katika ndoa za mapema.

Katika kongamano lililoandaliwa na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu ikiwemo Equality Now pamoja na Sauti ya Wanawake, lililojumuisha vijana katika kaunti ya Kwale,vijana wamedai kwamba hawajahusishwa kikamilifu katika mchakato wa kupambana na dhulma za kijinsia katika kaunti hiyo.

Kulingana na Dina Otieno kutoka shirika la sauti ya wanawake kutoshirikishwa kwa vijana katika  mchakato wa kukabiliana na visa vya dhulma za kijinsia kumechangia kuongezeka kwa visa hivyo katika kaunti ya Kwale

Aidha athari za ugonjwa wa korona nchini limetajwa kama  changio kubwa katika dhulma za kijinsia miongoni mwa watoto.

By Gladys Marura