AfyaHabariMombasa

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amesisitiza haja ya wananchi kujitolea kutoa damu…

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amesisitiza haja ya wananchi kujitolea kutoa damu ili kukabiliana na changamoto za upungufu wa damu katika hosipitali mbali mbali nchini.

Akizungumza wakati akiunga mkono hoja iliyowasilishwa bungeni na kamati ya Afya kuhusiana na maswala ya ukusanyaji wa damu Abdulswamad amewapongeza baadhi ya wakenya wanaojitolea kukusanya damu kama njia moja wapo ya kuwasaidia baadhi ya wagonjwa wenye mahitaji ya damu.

Kufuatia hayo Abdulswamad anawahimiza wakenya kujiunga na shirika la Redsplash katika juhudi za kukabiliana na changamoto za uhaba wa bidhaa hio muhimu nchini.

Aidha amelipongenga shirika hilo kwa kuja na mpango  ambapo wengi wamejisajili hatimae kuwarahisishia wengi katika kukusanya damu.

Haya yanajiri huku shirika hilo likikusanya panti za damu takrbani elfu 5 kila mwaka.

BY NEWS DESK