Habari

Kijana mmoja auawa kwa kukatwa na panga katika  kata ndogo ya Taru eneo la Mackinnon Road katika eneo bunge la kinango………….

Kijana mmoja auawa kwa kukatwa na panga na wenzie katika  kata ndogo ya Taru eneo la makinon katika eneo bunge la kinango kaunti ya kwale baada ya kushiriki katika mapigano na vinjan wenzake huki kiini cha vita hivyo kufikia sasa bado haijajulikana.

Akizungumza na meza yetu ya habari katika mahojiano ya kipkee kupitia njia ya simu mkuu wa kitengo cha usalama eneo hilo. Ibrahim Nyamae amesema kuwa kijana huyo  aliaga dunia alipokuwa akikimbizwa hosipitali baada ya kukatwa na panga kwenye vita hiyo ambayo kufikisasa hajaibainika ili leletwa na nini.

Kadhalika ameongeza kuwa tayari kamati ya usalama eneo hilo limeshaandaa mkutano wa kuleta pamoja wakazi pamoja na vijana ili kudumisha amani n ahata kubaini kiini cha vita hivyo. Huku akisema kuwa ni mara ya kwanza vurugu kama hizo kushuhudiwa katika eneo hilo.

 

By David Otieno