Ajuza mmoja kutoka kijiji cha Muyeye viungani mwa mji wa Malindi sasa anakila sababu ya kutabasamu baada ya kupokea ufadhili wa nyumba kutoka kwa shirika moja eneo hilo.
Akizungumza baada ya kupokea nyumba hiyo Ajuza huyo kwa jina Rehema Sharrif anasema kwa muda sasa amekuwa akiishi bila nyumba baada ya mmewe kuaga dunia miaka mingi iliyopita.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 75 amebainisha kuwa kwa sasa anategemea kuvunja kokoto ili kulisha wajuu wake anaoishi nao kwenye kipande chake cha ardhi.
Wakati uohuo mmoja wa wahisani hao Maimuna Farouk amesema kuna haja yabwahisani zaidi kujitokeza na kutoa msaada kwa wakaazi wengi anaosema wanaishi katika hali ya uchochole.
Maimuna anasema wengi wa wakaazi waoishi katika vitongoji wanahitaji msaada wa dharura akitoa changamoto kwa viongozi kujitokeza na kunusuru maelfu ya wakaazi wanaohangaishwa na baa la njaa kwa sasa.
Ujenzi wa nyumba hio uliofadhiliwa na shirika la Helping Hand uligarimu kima cha shilingi laki mbili.
By Malindi Correspondet