HabariMazingira

Mshukiwa wa Al-shabaab auawa huko Liboi mpakani mwa Garissa

Mshukiwa wa ugaidi wa kundi la Al-shabaab ameuawa baada ya maafisa wa polisi kumkamata punda aliyekuwa amebeba bunduki mbili aina ya AK47, vifaa vya kutengeneza mabomu katika mpaka wa Liboi kaunti ya Garissa.

Maafisa walioongoza oparesheni hiyo wamesema mshukiwa ambaye alikuwa na punda huyo aliuliwa kwa kupigwa risasi baada ya kukosa kujisalimisha, na inaaminika kwamba alikuwa akilekea mjini Garissa.

Kamishna wa eneo la kaskazini mashariki Nicodemus Ndalana anasema kwamba magaidi hao wamekuwa wakitumia mbinu mpya ya kusafirisha silaha kwa kutumia punda.

 

By Warda Ahmed