HabariSiasa

MABWENYENYE KAUNTI YA KWALE WAONYWA………

Waziri wa ardhi kaunti ya Kwale Saumu Mahaja amewaonya vikali mabwenyenye dhidi ya unyakuzi wa ardhi ya umma katika kaunti hiyo.

Akizungumza huko mjini Kwale, Mahaja ametoa onyo hilo kwa mabwenyenye wanaotumia nguvu kunyakua mashamba ya wakaazi.

Waziri huyo sasa anawataka mabwenyenye hao kuzingatia sheria katika mchakato wa kukodisha upya ardhi ya umma.

Hata hivyo, Mahaja amesema kwamba serikali ya kaunti ya Kwale inazifuatilia kwa ukaribu kesi zinazohusu mizozo ya ardhi.

Waziri huyo ameeleza kuwa wanalenga kuhakikisha wakaazi waliodhulumiwa mashamba yao kaunti hiyo wanapata haki mahakamani.

 

BY REPORTER