AfyaHabariSiasa

KAUNTI YA KWALE YAFAIDIKA NA MIRADI YA MAENDELEO

Gavana wa Kwale Salim Mvurya amesema kuwa kaunti hiyo imefaidika pakubwa na miradi ya maendeleo iliyoanzishwa chini ya mpango wa ruwaza ya mwaka wa 2030. 

Mvurya amesema kuwa mradi wa bwawa la Mwache ni kati ya miradi inayotekelezwa chini ya mpango huo katika eneo bunge la Kinango. 

Gavana huyo amesema kwamba ujenzi wa barabara ya Dongo Kundu ni mradi mwingine unaolenga kufungua uchumi katika eneo la Kusini mwa Pwani. 

Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa ruwaza ya mwaka wa 2030 James Mwangi amesema kuwa barabara hiyo inajengwa kupitia ushirikiano na gavana Mvurya. 

Mwangi ambaye pia ni afisa mkuu mtendaji wa benki ya Equity amesema kukamilika kwa mradi huo kutaimarisha biashara katika kaunti hiyo.

 

 

BY BINTIKHAMIS MOHAMMED