Serikali imeweka mkakati mpya wa kudhibiti ugonjwa wa korona unaoendelea kuwahangaisha wananchi kwa miezi 15 sasa tangu kisa cha kwanza kuripotiwa nchini.
Rais Uhuru Kenyatta anataka kueka kenya katika ligi ya mataifa yaliyodhibiti ugonjwa huu, badhi ya mataifa hayo yakiwemo Australia,Israeli ,New Zealand, Monaco, Iceland, Djibouti na kisiwa cha Solomon.
Katika mkakati wa wizara ya afya ni kuwa ifikapo mwezi juni mwaka wa 2022 kenya itakua inarikodi asilimia ndogo zaidi ya maambukizi .
Mwenyekiti wa chama cha ushauri ya utoaji chanjo nchini Wilis Akhwale amesema kuwa serikali itaongeza kasi ya chanjo.
Akizungumza na kituo kimoja cha habari Akhwale amesema kuwa serikali inampango wa uzalishaji wa chanjo si za korona pekee bali za magonjwa yote kama vile magonjwa ya watoto kama vile polio.
BY REPORTER