AfyaHabari

SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KUDHIBITI UGONJWA WA KORONA

Serikali imeweka mkakati mpya wa kudhibiti ugonjwa  wa korona  unaoendelea kuwahangaisha wananchi kwa miezi 15 sasa tangu kisa cha kwanza kuripotiwa nchini.

Rais Uhuru Kenyatta  anataka kueka kenya katika ligi ya mataifa yaliyodhibiti ugonjwa huu, badhi ya mataifa  hayo yakiwemo Australia,Israeli ,New Zealand, Monaco, Iceland, Djibouti na kisiwa cha Solomon.

Katika mkakati wa wizara ya afya ni kuwa ifikapo mwezi juni mwaka wa  2022 kenya itakua inarikodi asilimia ndogo zaidi ya maambukizi .

Mwenyekiti wa chama cha ushauri ya utoaji chanjo nchini  Wilis Akhwale  amesema kuwa serikali itaongeza kasi ya chanjo.

Akizungumza na kituo kimoja cha habari Akhwale amesema kuwa serikali inampango wa uzalishaji wa chanjo si za korona pekee bali za magonjwa yote kama vile magonjwa ya watoto kama vile  polio.

 

BY REPORTER