Habari

TUME YA HUDUMA ZA WALIMU TSC KUFANYA MKUTANO NA WANACHAMA WA KNUT

Tume ya huduma za walimu TSC imekubali takwa la chama cha kitaifa cha walimu KNUT la TSC kufanya mkutano mwingine na wawakilishi wa chama hicho ili kujadili kuhusu mkataba wa maelewano baina yao na walimu wa mwaka wa 2021/25

July mosi KNUT ilikataa mapendekezo ya TSC kuhusu kutekelezwa kwa mkataba huo vilevile nyongeza ya mishahara kwa wanachama wake na walimu ikitaka TSC kuitisha mnkutano mwingine.

Katika notisi afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia ameiandikia KNUT kupitia katibu mkuu mpya Collins Oyuu kuhusu mkutano huo utakaofanyika tarehe 13 mwezi huu.

Macharia amesema ajenda kuu za mkutano huo ni yaliyoafikiwa katika mkutano wa awali, kujadiliana kuhusu mkataba wa mwaka 2021/25 vilevile kutia saini mkataba huo unaolenga kuwaongezea walimu mshahara na marupurupu

 

BY JOYCE MWENDWA