Serikali ya kaunti ya Kilifi imesema itashirikiana na wazee wa kaya ili kuhakikisha inahifadhi misitu ya Kaya.
Kulingana na naibu gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Saburi, misitu hiyo kwa sasa inavamiwa na kukata kwa minajili ya kufanywa kuwa makazi ya watu, hali anayoitaja kuwa kinyume cha mila za tamaduni za jamii ya mijikenda.
Akiongea wakati wa maombi ya amani kwa ajili ya kuleta mvua katika Kaya Ribe, Saburi amesema wazee wa kaya wanafaa kuheshimiwa pamoja na utamaduni wa mijikenda kuheshimiwa.
Kwa upande wake mshirikishi wa muungano wa wazee wa Kaya za mijikenda Tsuma Nzai amezitaka jamii zote za mijikenda kushirikiana ili weweze kufuata tamaduni na mila ya jamii hiyo.
Aidha Nzai ameitaka serikali kuu na ile ya kaunti ya Kilifi kuhakikisha wanatoa hatimiliki kwa misitu hiyo .
Maombi hayo yanayofanyika katika kila msitu wa Kaya ukanda wa pwani yanatarajiwa kukamilika Julai 23.
By News Desk